Watu 10 wauwawa katika mashambulizi ya Israel, Gaza
11 Aprili 2025Msemaji wa Wakala wa ulinzi wa umma katika Ukanda wa Gaza, Mahmud Bassal ameliambia shirika la habari la AFP kwamba maiti za watu kumi wa familia moja, wakiwemo watoto saba zimepelekwa katika hospitali moja katika eneo la kati ya mji. Shambulizi hilo liliilenga nyumba ya familia ya Farra katika mji wa Khan Yunis.
Mapema leo jeshi la Israel limetoa amri nyingine inayowataka wakaazi waondoke kutoka kwenye maeneo kadhaa ya Mashariki mwa mji wa Gaza.
UN yaonya kuhusu amri zinazotolewa na Israel kwa Wapalestina wa Gaza
Ripoti ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeonya kwamba kuongezeka kwa amri zinazotolewa na jeshi la Israel kuhusu wapalestina kuhama kutoka kwenye maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza , ni sawa na kuwahamisha kwa lazima na kuliacha eneo la Ukanda waGaza kuendelea kuwa dogo kutokana na kwamba maeneo wanayohamishwa yanatengwa kama maeneo ya usalama chini ya serikali ya Israel.
Umoja wa Mataifa umesema hali hiyo inaibua wasiwasi iwapo itawezekana hapo baadaye kwa Wapalestina kuendelea kuishi Gaza.
Watu 23 wauawa kufuatia shambulio la Israel katika jengo la makaazi ya watu Gaza
Na Saudi Arabia imetaka shinikizo zaidi ili kuhakikisha upelekaji wa misaada unaendelea bila kutatizwa katika Ukanda wa Gaza baada ya Israel ya kuzuia uingizaji wa mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Hayo yamesemwa Ijumaa na waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan baada ya mkutano wa kikanda wa washirika uliofanyika kusini mwa Uturuki.