Watu 10 wauwawa baada ya tukio la kufyatuliwa risasi Sweden
5 Februari 2025Mtu huyo aliyejihami ni miongoni mwa waliofariki. Tukio hilo limeelezewa na waziri mkuu wa Sweden Ulf Kristersson kama tukio baya zaidi la ufyatuaji wa risasi kwa halaiki ya watu katika historia ya nchi hiyo. Idadi kamili ya watu waliouwawa bado haijabainika.
Tukio hilo limefanyika nje ya mji wa Orebro, mji ulio karibu kilomita 200 magharibi mwa Stockholm. Kituo hicho cha elimu kinatoa elimu kwa wanafunzi walio zaidi ya umri wa miaka 20.
Soma pia: Sweden yajiunga na NATO na kuwa mwanachama wa 32
Mamlaka za Sweden zinasema tukio hilo si la kigaidi ila hazikutoa sababu ya shambulizi hilo.
Matukio ya mashambulizi ya bunduki nchini Sweden ni nadra ila katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa matukio kadhaa ambapo watu walijeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa visu au shoka.