Watu 10 wauwa nchini Israel kutokana na mashambulizi ya Iran
15 Juni 2025Polisi ya Israel imesema watu sita wameuawa na takriban 180 kujeruhiwa katika eneo la mashambulizi huko Bat Yam, karibu na Tel Aviv kwenye pwani ya Mediterania nchini Israeli.
Maafisa wa uokoaji waliovalia kofia za kinga na taa za kichwa, waliendeleza juhudi za kutafuta manusura.
Askari 7 wa Israel wajeruhiwa, huku wanasayansi watatu wa Iran wakiuawa
Katika hatua nyingine, Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kuwa nchi yake haijahusika kivyovyote na kampeini kali ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran iliyoanza siku ya Ijumaa.
Pia, kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump, ametishia kuchukuwa hatua kali ikiwa Iran itashambulia maslahi ya Marekani.
Hata hivyo, rais huyo ameongeza kuwa wanaweza kupata makubaliano kwa urahisi kati ya Iran na Israel kumaliza mzozo huo hatari.