MigogoroUlaya
Watu 10 wauawa katika mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine
18 Agosti 2025Matangazo
Shambulio hilo la kwanza la droni lilililenga eneo la kaskazini mashariki mwa Kharkiv. Katika tukio hilo watu wengine saba waliuawa. Katika shambulio jingine la kombora watatu wameuawa kusini mashariki mwa Zaporizhzhia.
Gavana wa eneo hilo amesema watu 23 wamejeruhiwa. Mashambulizi hayo yamejiri zikiwa zimesalia saa chache kabla ya mkutano wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Rais wa Marekan Donald Trump unaolenga kuvimaliza vita kati ya Urusi na Ukraine.
Rais Zelensky ameyalaani mashambulizi hayo akisema Rais wa Urusi Vladimir Putin anafanya mauaji hayo ili kuendelea kuishinikiza Ulaya na Ukraine pamoja na kuzidharau juhudi za kidiplomasia.