Watu 10 wameuawa Kenya wakati wa maandamano ya Julai 7
8 Julai 2025Takriban watu 10 wameuawa nchini Kenya na mamia kukamatwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali siku ya Jumatatu, shirika la kutetea haki za binadamu nchini humo limesema.
Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya imelishutumu jeshi la polisi kwa kushirikiana na magenge ya wahalifu wakati wa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji katika viunga vya mji mkuu Nairobi.
Msemaji wa Polisi ya Kitaifa Kenya, Michael Muchiri ameikosoa taarifa hiyo ya tume ya haki na kusema kwamba haina ukweli lakini akaweka wazi kwamba watu 567 wamekamatwa wakati wa maandamano hayo.
Vijana wa kenya walipanga kufanya maandamano Julai 7 kulalamikia ukatili wa polisi dhidi yao, rushwa, uchumi mbaya, kupanda kwa gharama ya maisha na kumtaka pia rais William Ruto kuondoka madarakani.