Watu 10 wafariki kutokana na mafuriko mjini Karachi
21 Agosti 2025Matangazo
Vifo hivyo vinasemekana kusababishwa na watu kuzama maji, ajali za barabarani, kuanguka kwa majengo na kufariki kutokana na kupigwa na umeme.
Mvua zaidi inatazamiwa kunyesha nchini humo. Mvua hiyo ilianza kunyesha Jumanne na kufikia viwango ambavyo havijashuhudiwa kwa miaka katika maeneo ya kusini ya mji huo ambao ni makao ya watu zaidi ya milioni 20.
Mvua hizo zimesababisha athari kubwa kote nchini Pakistan katika siku chache zilizopita huku idadi ya vifo kutokana na mafuriko yaliyolikumba eneo la milimani la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ikiongezeka na kufikia watu 385 kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita.