Watoto waliozaliwa kwa IVF kutorithi magonjwa ya mama zao
17 Julai 2025Matangazo
Watoto wanane wenye afya nzuri wamezaliwa nchini Uingereza kwa kutumia mbinu mpya ya upandikizaji wa mimba (IVF) ambayo imefanikiwa kupunguza hatari ya kurithi magonjwa ya vinasaba DNA kutoka kwa mama zao.
Matokeo hayo yameelezwa kuwa ni mafanikio makubwa yanayotoa matumaini kwamba wanawake wenye magonjwa ya kurithi wanaweza siku moja kupata watoto bila kuwarithisha magonjwa watoto wao.
Mnamo mwaka 2015, Uingereza ilikuwa nchi ya kwanza kuidhinisha mbinu ya IVF inayotumia kiasi kidogo cha vinasaba vyenye afya kutoka kwa yai la mchangiaji pamoja na yai la mama na mbegu ya baba.