MigogoroMashariki ya Kati
Watoto 8 wameuawa wakisubiri huduma ya maji Gaza
14 Julai 2025Matangazo
Jeshi la Israel limedai kuwa "tatizo la kiufundi" katika shambulio lililokuwa likimlenga mwanachama wa kundi la Islamic Jihad ambalo ni mshirika wa Hamas ndilo lililosababisha mauaji hayo. Katika shambulio hilo watu zaidi ya 17 wamejeruhiwa.
Katika Shambulio jingine shirika la habari la Palestina limesema Mshauri wa hospitali ni mmoja wa watu 12 waliouawa katika shambulio la anga lililotua kwenye soko lenye shughuli nyingi katikati mwa Gaza. Jeshi hilo limeongeza kuwa mashambulizi lililoyafanya kwa saa 24 zilizopita yalilenga zaidi ya miundombinu 150 ya kigaidi kote kwenye ukanda huo.