SiasaUkraine
Watatu wauawa Urusi kufuatia mashambulizi ya Ukraine
11 Agosti 2025Matangazo
Meya wa Moscow Sergei Sobyanin amesema hayo Jumatatu kupitia ukurasa wake wa Telegram.
Wakati huo huo, wizara ya Ulinzi ya Urusi, imesema watu watatu wameuawa kufuatia mashambulizi hayo ya droni ya Ukraine yaliyolenga majimbo ya Tula, Nizhny Novgorod na vilevile mji mkuu Moscow.
Kulingana na jeshi la Urusi, lilidungua droni 39 za Ukraine yaliyolenga maeneo mbalimbali ya Urusi.
Maafisa wa Ukraine, wamesema mifumo yao ya ulinzi pia ilidungua droni 59 miongoni mya zaidi ya 70 zilizofyatuliwa na Urusi.
Kwa zaidi ya miaka mitatu, Ukraine imekuwa ikijilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Pande zote mbili zimekuwa zikitumia droni za kijeshi katika mashambulizi yao.