Watanzania waomboleza kifo cha kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis. Wanamkumbuka namna ambavyo amehimiza upendo, haki na kusisitiza kwake mazungumzo ya kumaliza migogoro kwenye maeneo ya machafuko na alivyopigania haki za binadamu na mazingira.