Wataalamu waonya juu ya baa la njaa Gaza
12 Mei 2025Matangazo
Shirika linalofuatilia hali ya usalama wa chakula katika Ukanda wa Gaza, limesema asilimia 22 ya idadi ya watu wa Ukanda huo wanakabiliwa na hali mbaya ya janga la kibinadamu.
Shirika hilo limetahadharisha kwamba Gaza iko katika kitisho kikubwa cha kutumbukia kwenye baa la njaa.Soma pia: Mpango wa Marekani juu ya misaada ya kiutu Gaza wapingwa
Ripoti iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya shirika la IPC imesema wakaazi kiasi milioni 2.4 wa Gaza wako hatarini kukosa kabisa chakula au hata kutumbukia kwenye hali mbaya zaidi ya Baa la Njaa kufikia mwezi Septemba.
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limetowa mwito wa kuondolewa mara moja kwa vizuizi vilivyowekwa na Israel.