Sheria na HakiMashariki ya Kati
UN yaituhumu Israel kwa unyanyasaji wa kingono Gaza
13 Machi 2025Matangazo
Israel imekanusha vikali madai hayo na kusema tume hiyo ina upendeleo kwa kuitazama nchi hiyo kwa jicho tofauti na Palestina.
Kifaya Khraim ni mratibu wa shirika la kimataifa katika kituo cha kuwasaidia na kutoa ushauri nasaha kwa wanawake,alifafanua baadhi ya unyanyasaji uliotajwa.
Soma pia:Wahuthi wa Yemen wanuia kuanza tena kuzishambulia meli za Israel
Ripoti ya tume ya wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo Alhamisi inasema visa vya unyanyasaji wa kingono na unyanyasaji wa kinjinsia vimeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwa hali ya kutisha kwa Wapalestina.
Visa vilivyoorodheshwa ni pamoja na ubakaji, unyanyasaji wa kingono ikiwemo matukio ya watu kulazimishwa kuvua nguo hadharani.