050809 Porträt Steinmeier BTW HF
14 Septemba 2009Septemba 27 Wajerumani hawapigi kura kumchagua kansela wao bali ni bunge jipya linalochaguliwa. Hata hivyo uchaguzi huo una muhimu mkubwa kwa wagombea ukansela wanaowakilisha vyama vikuu. Kwanza yupo Kansela Angela Merkel anaependwa na Wajerumani. Vile vile kuna mpinzani wake: mgombea ukansela wa chama cha SPD Frank-Walter Steinmeier. Yeye anakiongoza chama cha SPD katika uchaguzi huku uchunguzi wa maoni ukionyesha kuwa umaarufu wa chama hicho umefifia sana.
FRANK-WALTER STEINMEIER
"Kigogo bila yeye mwenyewe kutaka" ndio Naibu Kansela "Frank-Walter Steinmeier alivyoitwa na gazeti la "Welt am Sonntag" Juni mwaka 2008. Wakati huo alionekana kana kwamba asingependa kuingia katika king´anyiro cha ukansela kwa tiketi ya chama chake cha SPD. Hata hivyo miezi minne baadaye mnamo mwezi wa Oktoba 2008 sura yake ilionekana kwenye mabango ya SPD. Alichaguliwa na wajumbe wa SPD kwa asilimia 95 kutoa changamoto kwa kansela anayependwa Angela Merkel.Na alipozungumzia juu ya hatua hiyo Steimeier alisema
"Nimepima na wala sikupitisha uamuzi bila ya kufikiria. Na ninasema ikiwa mnaniamini basi ndugu mimi nipo tayari"
Kwa hatua hiyo Steinmeier alijitokeza kutoka mstari wa nyuma
HISTORIA YAKE
Kwa kweli Steinmeier alikawia kuingia katika uwanja wa kisiasa. Azaliwa Januari 5 mwaka 1956 mjini Detmold na alikulia katika kijiji cha Brakelsiek na akasomea sheria na siasa. Baada ya kumaliza masomo yake alifanyakazi kama mtaalamu katika ofisi ya serikali mjini Gießen na alikuwa pia mhadhiri mjini Wiesbaden.
Baada ya kuingia katika chama cha SPD hapo mwaka 1975,Steinmeier alikwenda kufanya kazi katika ofisi ya serikali ya jimbo la Niedersachsen kama mshauri wa haki na sera za vyombo vya habari. Alipewa wadhifa huo na Waziri Mkuu wa zamani wa jimbo hilo Gerhard Schroeder.Binafsi wakati huo Steimeier alipopewa nafasi hiyo alisema.
IMANI
Punde si punde Steinmeier alipata imani ya Schroeder na akawa kiongozi wa ofisi yake na katika mwaka 1998 chama cha SPD kiliposhinda uchaguzi mkuu, Steinmeier aliondoka Hannover pamoja na Schroeder na walifuatana hadi Bonn na baadaye mjini Berlin.
Miongoni mwa majukumu aliyokuwa nayo kama katibu wa dola katika ofisi ya kansela ni kuratibu shughuli za idara ya ujasusi.Mwaka 1999 akawa mkuu wa ofisi ya kansela,wadhifa aliyoendelea kushika baada ya serikali ya mseto ya vyama vya SPD na Kijani kushinda kwa akura chache uchaguzi wa mwaka 2002.
Steinmeier akashika wadhifa wa waziri wa mambo ya nje kufuatia uchaguzi wa Septemba 2005 uliyoitishwa mapema - na Schroeder aliyekuwa rafiki yake, kuondoka katika jukwaa la kisiasa.
Kwa haraka aliwavutia Wajerumani na akapata imani yao kwa kiwango cha kutokeza kama mwanasiasa maarufu kabisa hata kuliko Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, mwaka mmoja tu baada ya kushika wadhifa huo.
UMAARUFU WASHUKA
Chama cha SPD Juni mwaka huu kiliingia katika kampeni ya uchaguzi kikijikuta kuwa kimepoteza umaarufu wake kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa na chama hicho. Mgombea ukansela wa SPD alionekana kana kwamba ameishiwa na nguvu hata kabla ya kinyanganyiro cha uchaguzi kushika kasi. Lakini juma moja kufuatia uchaguzi wa Ulaya, Steinmeier ghafula aliibuka katika mkutano mkuu wa SPD kwa kutoa hotuba ya kusisimua.
Steinmeier alishangiliwa kwa dakika kumi nzima na chama chake kikamshukuru kwa kukipatia matumaini makubwa katika wakati huu mgumu kuelekea uchaguzi mkuu.
Mwandishi: B.Marx/ZPR/P.Martin
Mhariri:Mohamed Abdul-Rahman