Ni wasichana watatu walioamua kuwaelimisha wengine namna ya matumizi ya akili bandia katika kutafuta suluhu za changamoto zinazoikumba jamii. Si rahisi kwao kueleweka, kutokana na ushiriki mdogo wa wasichana katika masuala ya teknolojia, lakini bado wanajivunia kuwa sehemu ya mafanikio kwa baadhi ya walioamua kujitokeza.