Washutumiwa wa Taliban wauawa Afghanistan:
6 Machi 2004Matangazo
KABUL: Nchini Afghanistan wanajeshi wa Kimarekani wamewapiga risasi na kuwauwa washambuliaji tisa wakati wa operesheni zao za kijeshi. Msemaji wa jeshi alisema, washambuliaji wapatao 30 - 40 walijaribu kuwaingiza mtegoni wanajeshi wapatao 10 wa Kimarekani. Haikudhihirika nani alishambulia mwanzo. Inasemekana hakuna wanajeshi wa Kimarekani waliouawa au kujeruhiwa. Wiki iliyopita wanajeshi wa Kimarekani walimpiga risasi na kumwua mwanagambo wa Kiafghani mkoani Paktika unaosemekana ni ngome mojawapo ya wanamgambo wa Taliban na Al Qaida. Upande wa pili wa mpaka wanajeshi wa Kipakistani wanaendeleza operesheni zao za kuwatafuta wanachama wa itikadi kali wa Al Qaida.