Washutumiwa wa Taliban wauawa Afghanistan:
7 Machi 2004Matangazo
KABUL:
Nchini Afghanistan wanajeshi wa Kimarekani
wamewapiga risasi na kuwauwa washambuliaji tisa
wakati wa operesheni zao za kijeshi. Msemaji wa
jeshi alisema, washambuliaji wapatao 30 - 40
walijaribu kuwaingiza mtegoni wanajeshi wapatao
10 wa Kimarekani katika mkoa wa Paktia kwenye
eneo la mpaka wa Pakistan. Katika eneo hilo
wanajeshi 13,000 chini ya uongozi wa Marekani
wanafanya operesheni za kuwatafuta wafuasi wa
Taliban na Al Qaida. Wiki iliyopita wanajeshi
wa Kimarekani walimpiga risasi na kumwua
mwanagambo wa Kiafghani mkoani Paktika
unaosemekana ni ngome mojawapo ya wanamgambo wa
Taliban na Al Qaida. Upande wa pili wa mpaka
wanajeshi wa Kipakistani wanaendeleza
operesheni zao za kuwatafuta wanachama wa
itikadi kali wa Al Qaida.