Washutumiwa 300 watiwa nguvuni Iraq:
23 Novemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Nchini Iraq wanajeshi wa mwungano wamekwisha watiwa nguvuni washutumiwa 300 wa kigaidi, wengi wao wanasemekana wanatokea nchi za Kiarabu. Sehemu yao kubwa wanatokea Syria na Iran, alisema msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani mjini Baghdad. Mara kwa mara, Marekani na Uingereza zimezishutumu Syria na Uiran kuingiza wapiganaji wa chini kwa chini Iraq. Shutuma hizo zimepinga na serikali za Damaskus na Teheran.