Washiriki kadhaa wasusia hotuba ya Urusi: UN
26 Februari 2025Matangazo
Washiriki hao ni pamoja na balozi wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, na kukusanyika nje ya chumba ambako kikao cha maadhimisho ya miaka mitatu ya uvamizi wa Urusi nchini humo kilikuwa kikiendelea.
Balozi wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa Simon Manley ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba uungaji wao mkono kwa Ukraine ni thabiti na kusisitiza wanataka kuona amani ya haki na ya kudumu itakayowiana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.
Kiti cha Marekani kwenye Baraza hilo kilikuwa wazi kufuatia hatua ya Rais Donald Trump kujitoa kwenye chombo hicho, ambacho ni pekee cha kimataifa cha kulinda haki za binaadamu.