WASHINTON: Zalmay Khalilzad balozi mpya wa marekani nchini Iraq
6 Aprili 2005Matangazo
Rais Gorge Bush amechagua Zalmay Khalilzad kuwa balozi wa Marekani nchini Iraq.
Khalilzad ambye ni balozi wa sasa nchini Afghanstan atachukua mahala pa John Neroponte ambaye anachukua wadhifa wa mkurugenzi wa idara ya usalama nchini Marekani.
Baada ya utezi huo kupitishwa na bunge Khalilzad ambaye ni muafghantan aliyezaliwa Marekani ataongoza wadhifa mgumu zaidi wa kibalozi duniani.
Hata hivyo balozi huyo mwenye umri wa miaka 54 ameahidi kushirikiana na wairaq wote ili afanikishe lengo la kupatikana mafanikio nchini Iraq.