WASHINGTON:Waziri Mkuu wa China yuko Marekani
8 Desemba 2003Matangazo
Waziri Mkuu wa China Wen Jiabao amewasili nchini Marekani kuanza ziara yake ya siku nne. Tayari amekuwa na mkutano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan mjini New York ambao Annan ameuelezea kuwa wa manufaa sana na wa kuchangamsha.Ameongeza kusema kwamba mazungumzo yao yamelenga uhusiano wa China na Umoja wa Mataifa,Iraq,suala la Korea na jitihada za kudhibiti UKIMWI na virusi vya HIV.Rais George W Bush wa Marekani atamkaribisha Wen katika Ikulu ya Marekani mjini Washington hapo kesho. Kiongozi huyo wa China pia ataitembelea Canada,Mexico na Ethiopia.