WASHINGTON:Wanajeshi wa Marekani washutumiwa kukiuka sheria Iraq
15 Oktoba 2005Matangazo
Afisa mkuu katika Umoja wa Mataifa amewashutumu wanajeshi wa Marekani nchini Iraq kwa kukiuka sheria ya kimataifa kwa kuzuia kimakusudi chakula na maji kwa wairaq.
Mchunguzi wa haki za binadamu Jean Ziegler amesema wanajeshi wa Marekani walitumia ujanja huo ili kuwatoa watu majumbani mwao kwenye miji iliyo ngome za waasi kufuatia operesheni zao za kijeshi.
Hata hivyo wanajeshi wa Marekani wamekanusha madai hayo lakini wamekiri kwamba usambazaji wa chakula ulitatizwa mara kwa mara katika operesheni za kijeshi.