WASHINGTON:Marekani yapuuza wito wa Russia wa kuitaka iondoshe wanajeshi Iraq
19 Agosti 2005Matangazo
Marekani imekataa kuitikia mwito war ais Vladmir Putin wa kuitaka kutoa ratba ya kuondoa wanajeshi wake nchini Iraq.
Miezi 28 baada ya kumuondoa Saddam Hussein madarakani wanajeshi zaidi ya laki moja wa marekani wanaendelea kupambana na waasi hadi pale vikosi vya usalama vya Iraq vitakapoweza kujisimamia.
Rais Bush amekataa katakata kuweka tarehe ya kuwaondosha wanajeshi wake Iraq.Rais Putin pia amependekeza mkutano wa kimataifa kujaribu kuimarisha Iraq jambo ambalo Marekani haikusema lolote juu ya hilo.