WASHINGTON:Marekani kuendelea kuinga mkono serikali ya Iraq
1 Oktoba 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice amesema Marekani haipasi kuliacha jukumu lake nchini Iraq.
Rice ameonya kwamba kwa Marekani kuondoka nchini Iraq kutasababisha kuongezeka kwa maadui wa demokrasi na uhuru katika eneo la mashariki ya kati.
Nchini Iraq kwenyewe zikiwa zimebakia wiki mbili kuelekea kura ya maoni juu ya katiba mpya waasi wanaendelea kufanya hujuma zao dhidi ya raia na polisi.
Idadi ya watu waliouwawa katika kipindi cha siku mbili imefikia watu 110 kufuatia mashammbulio ya mabomu yanayofanyika kote nchini humo.
Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld amekanusha ripoti kwamba wanajeshi wa Iraq bado hawajaweza kukabiliana na mashambulio ya waasi nchini humo.