WASHINGTON:Maandamano kupinga uvamizi wa Iraq
20 Machi 2005Miaka miwili baada ya Iraq kuvamiwa na Marekani,wafanya maandamano wanaopinga vita walimiminika kwa elfu na elfu katika miji ya Ulaya.Maandamano makubwa kabisa yalifanywa katika mji mkuu wa Uingereza London ambako kiasi ya watu 50,000 waliandamana.Maandamano mengine makubwa yalifanywa katika miji ya Roma,Athens na Istanbul.Nchini Marekani maandamano ya amani yalifanywa katika mji wa New York.Kama watu 5,000 walikusanyika Central Park.Na rais George W.Bush wa Marekani alietoa amri ya kuivamia Iraq miaka miwili iliyopita,ameutetea uamuzi huo katika hotuba yake ya kila wiki kwenye redio.Amesema kwa sababu ya vita hivyo sasa kuna usalama zaidi nchini Marekani.Vile vile akasema kuwa vita hivyo vimeanzisha mageuzi ya kidemokrasia katika eneo la Mashariki ya Kati.