WASHINGTON:Hali ya Iraq yatia wasiwasi
22 Julai 2006Matangazo
Rais Gorge W Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki wiki ijayo watatafuta njia za kukubaliana juu ya kuimarisha usalama katika mji wa Baghdad.
Waziri mkuu al Maliki atasafiri kwenda mjini Washington Marekani kukutana na rais Bush siku ya Jumanne.
Nchini Iraq mapigano yameongezeka kati ya washia na wasunni na kuzusha hofu zaidi juu ya kutokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Kamanda wa cheo cha juu wa Marekani katika eneo la mashariki ya kati amesema hapo jana ijumaa kwamba kuongezeka kwa mapigano ya kimadhehebu mjini Baghdad kumezusha wasiwasi zaidi kuliko mashambulio ya waasi.