WASHINGTON:BUSH AFANYA ZIARA YA SIRI IRAQ
28 Novemba 2003Matangazo
Rais George W Bush wa Marekani amerudi nyumbani nchini Marekani baada ya kuwa na ziara ya siri mjini Baghdad Iraq. Akiwa chini ya ulinzi mkali amekwenda Iraq hapo jana kusheherekea siku ya mapumziko ya jadi ya Kimarekani ya Kutowa Shukrani akiwa pamoja na vikosi vya nchi yake.Maafisa wa serikali ya Marekani wanasema ziara hiyo ilikusudia kuongeza morali ya wanajeshi.Ikulu ya Marekani ilitangaza habari za safari hiyo ya Bush baada ya ndege ya Rais ya Air Force One kuondoka Baghdad.Waandishi habari wachache tu waliruhusiwa kuandamana na Bush katika safari hiyo. Bush amekuwa Rais wa kwanza kabisa wa Marekani kuitembelea Iraq.