WASHINGTON : Zao la kasumba Afghanistan ni tishio
5 Machi 2005Matangazo
Kwa mujibu wa repoti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani uzalishaji wa zao la kasumba nchini Afghanistan unatowa tishio kubwa sana kwa utulivu duniani.
Repoti hiyo ambayo imetangazwa hapo jana imeonya kwamba nchi hiyo iko kwenye ukingo wa kuwa taifa la madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa repoti hiyo eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya kulima zao hilo la kasumba nchini Afghanistan limeongezeka na kufikia hekta 206,000 mwaka jana kutoka hekta 61,000 hapo mwaka 2003.