WASHINGTON: Waziri wa ulinzi wa Marekani aituhumu China
19 Oktoba 2005Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld kabla ya kuwasili ziarani nchini China,kwa mara nyingine tena ameituhumu serikali ya Beijing kuwa matumizi ya China kwa miradi yake ya ulinzi ni kubwa kuliko vile inavyotajwa.Rasmi matumizi ya kijeshi ya China mwaka huu ni Dola bilioni 30,lakini mnamo mwezi Juni,wizara ya ulinzi ya Marekani-Pentagon ilisema,idadi halisi inakaribia Dola bilioni 90.Rumsfeld amesema hatua hiyo inachochea shaka kuhusu nia za Uchina-madai ambayo yanakanushwa na China.Waziri Rumsfeld yupo China kwa majadiliano pamoja na Rais Hu Jintao.Ziara hii ya Rumsfeld inatangulia ziara iliyopangwa kufanywa na rais George W.Bush wa Marekani nchini China mwezi ujao.