WASHINGTON: Wamarekani wengi wataka vikosi vyao viondoke Iraq
19 Juni 2005Matangazo
Nchini Marekani mdahalo unaendelea juu ya suala la kupanga tarehe ya kuviondosha vikosi vya Marekani kutoka Iraq.Idadi ya majeruhi wa Kimarekani nchini Iraq ikiongezeka,uchunguzi wa maoni huonyesha kuwa idadi ya watu wanaomuunga mkono Rais George W.Bush na juhudi za vita,inapunguka sana.Uchunguzi uliofanywa na Times na CBS nchini Marekani na kutangazwa siku ya Ijumaa umeonyesha kuwa asili mia 51 ya watu wanaamini kuwa Marekani isingejiingiza Iraq na asili mia 45 wanaunga mkono uvamizi wa Iraq.Hivi karibuni,wabunge wengi wa Kimarekani,ikiwa ni kutoka vyama vyote viwili vya Democrats na Republicans,walitoa mwito kuwa vikosi vya Marekani vianze kurejeshwa nyumbani ifikapo Oktoba mwaka 2006.