WASHINGTON: Rais George W Bush wa Marekani ameipa Iran masharti ili uboreke uhusiano baina ya nchi mbili.
2 Januari 2004Matangazo
Akizungumza na waandishi wa habari TEXAS, Bush aliitaka serikali mjini Teheran itekeleze mageuzi ya kisiasa. Isitoshe iwakabidhi wafuasi wa mtandao wa kigaidi wa El Kaida waliyoko Iran, na ijitenge kabisa na mipango ya kutaka kuunda silaha za kinyuklia. Bush aliweka wazi msaada wa Marekani kwa wahanga wa tetemeko la ardhi, hauna maana uhusiano umeshaanza kuboreka. Hapo awali waziri wa kigeni wa Iran Kamal Kharrazzi alielezea kama ni hatua ya busara, kuregezwa kwa muda vikwazo ilivyoekwa Iran na Marekani. Kutokana na hatua hiyo Wairan wanaoishi Marekani wataweza kutuma misaada ya dharura kwa watu wao nyumbani - alitamka Kharrazi.