WASHINGTON : Pendekezo la Iran halikidhi madai
24 Agosti 2006Marekani imesema pendekezo la Iran kwa mazungumzo ya nuklea halikidhi madai ya Umoja wa Mataifa kwamba isitishe shughuili zake nyeti za nuklea.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Dana Perino amesema Marekani imekuwa ikichambuwa kwa hadhari pendekezo hilo la Iran na kujadili na serikali nyengine hatua zaidi zinazofaa kuchukuliwa.Perino alikuwa akizungumza siku moja baada ya Iran kuwasilisha jibu lenye utata kwa mpango wa mataifa makubwa wa vifuta jasho vya kiuchumi na kisiasa kwa lengo la kuishawishi serikali ya Iran kusitisha urutubishaji wa uranium.
Katika jibu lake hilo Iran imesema iko tayari kuwa na mazungumzo makini juu ya mpango wake wa nuklea lakini haikutaja tarehe ya mwisho Augusti 31 iliowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo kusitisha urutubishaji wa uranium au kukabiliwa na uwezekano wa kuwekewa vikwazo.