WASHINGTON : Mpiga debe dhidi ya vita vya Iraq na mamia wengine mbaroni
27 Septemba 2005Matangazo
Polisi imemkamata mpiga debe wa kupinga vita vya Iraq Cindy Sheehan na zaidi ya wanaharakti 300 wakiwa nje ya Ikulu ya Marekani hapo jana wakati serikali ikisisitiza kwamba kampeni hiyo inayoongezeka haitomyumbisha Rais George W Bush.
Sheehan mama wa mwanajeshi wa Marekani aliyeuwawa nchini Iraq mwaka jana alichukuliwa akiwa na mpingu za plastiki akiwa amesimama miongoni mwa umati mkubwa wa watu ambao walionywa kwamba watakamatwa.
Zaidi ya waandamanaji 500 walikusanyika karibu na lango kuu la jumba la Rais kila mmoja akiwa amebeba bango lenye jina la mwanajeshi wa Marekani aliyeuwawa nchini Iraq.